Translations:Policy:Universal Code of Conduct/8/sw

From Wikimedia Foundation Governance Wiki
Revision as of 04:23, 19 April 2024 by Kisare (talk | contribs)

Mwongozo huu wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (MUKIMUMA) unatoa tafsiri ya tabia inayokubalika na isiyokubalika katika harakati za shirika la Wikimedia. Mwongozo huu utatumika kwa kila mmoja ambaye kwa namna moja ama nyingine anahusika na uchangiaji wa maudhui katika miradi ya Wikimedia Foundation mtandaoni , nje ya mtandao au katika sehemu yoyote ambapo shughuli za Wikimedia zinafanyika. Mwongozo huu utafuatwa na wanawikimedia wote yaani wachangiaji wapya na wazoefu, vyombo mbalimbali vya utendaji katika miradi ya Wikimedia Foundation, wafanyakazi na wajumbe wa bodi. Mwongozo huu pia utatumika katika mikutano yote yaani ya ana kwa na ile ya mtandaoni, sehemu mbalimbali ambazo miradi ya Wikimedia itakuwa ikifanyika, katika miradi yote ya Wikimedia pamoja na katika Wiki (Wikipedia) zote.